• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bukombe yapitisha rasimu ya mpango wa bajeti 2019/2020

Imewekwa: February 21st, 2019

Kwa mwaka wa fedha  2019/2020  baraza maalumu la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti  yenye jumla ya Tshs 32,720,162,547.99 kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa mchanganuo ufuatao:- Mapato ya ndani Tshs. 1,990,902,999.99, Ruzuku kutoka serikali 26,896,279,461.00 na Miradi yamaendeleo (Ruzuku na Nguvu za Jamii) Tshs. 3,832,980,087.00 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 20 Februari, 2019.

Akisoma rasimu hiyo ya bajeti Afisa mipango wa Wilaya Sarah Yohana kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji alisema kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 1982 ya serikali za Mitaa kifungu cha 43 (1) kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa, inatakiwa kuandaa na kupitisha bajeti ya mapato na matumizi kwa muda usiopungua miezi miwili kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha.

Sarah alisema  uandaaji wa bajeti hiyo umezingatia mwongozo wa bajeti uliotolewa na serikali kupitia Wizara ya fedha, mahitaji muhimu ya Wilaya kulingana na mpango mkakati wa Halmashauri, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Tawala, Mpango wa maendeleo Endelevu, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano II 2021, Dira ya Maendeleo ya Taifa hadi 2025 na maelekezo ya viongozi wa juu wa Serikali. 

Aidha aliendea kusema kuwa mikakati ya utekelezaji wa bajeti  hiyo ni pamoja na kuendeleza matumizi ya mifumo ya kieletroniki  (POS) katika ukusanyaji wa vyanzo vya ndani vya mapato vya Halmashauri kama vile masoko, vituo vya kutolea huduma za afya, minada na maegesho, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa vyanzo vilivyopo na kuendeleza kubuni vyanzo vingine ili kuimarisha mapato ya Halmashauri, kuendeleza kuibua vyanzo vipya ambavyo havitegemei hali ya hewa na vinavyohitaji gharama kidogo za ukusanyaji kama vile mgodi, maduka ya madawa ya binadamu, mialo ya wachenjuaji wa dhahabu, ushuru wa madini ya ujezi kama vile kokoto, mawe na mchanga pamoja na tozo na adhabu na kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ambayo yataboresha utekelezaji wa bajeti.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Safari Mayala aliwataka waheshimiwa madiwani kupitia mapendekezo ya bajeti kwa umakini na kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri ili iwe  dira ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Kikao cha kupitisha rasimu ya mapendekezo ya bajeti kilikuwa cha siku mbili ambapo siku ya kwanza ilikuwa ni mapitio ya utekelezaji wa mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kuishia 31 Desemba , 2018 na siku ya pili ilikuwa ni kupitia  makisio ya mapato na matumizi ya mpango wa maendeleo wa Halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

UMISSETA BUKOMBE WAAHIDI KURUDI NA USHINDI
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa